Underplayed Gems
The whole movie catalogue

Films and series, searchable by what they are

← Back to the shop

Chumo (2011)

Chumo poster
Country
Tanzania

How it feels

A young Tanzanian couple faces family obstacles while in love. The story also shares a message about malaria during pregnancy.

romanticpoignantaccessibleeducationalearnestmelodramaticfamily-dramalow-budget

What happens

Chumo ni filamu iliyotoka mwaka 2011 nchini Tanzania. Ndani yake anakuja Hussein Mkiety (Juma), Jokate Mwegelo (Amina), Jafari Makati (Ali), Yusuph Mlela (Yustus). Filamu imetayarishwa na Tanzania na kufadhiliwa na JHU-CCP kupitia Mfuko wa Rais wa kutokomeza Malaria na USAID. Chumo inawasilisha ujumbe wa malaria wakati wa ujauzito kupitia hadithi ya kusisimua ya wapenzi wenye bahati mbaya. Wawili wanapendana lakini vikwazo vya kifamilia vinapelekea mapenzi yao kuwa magumu. Filamu imeongozwa na Jordan Riber ambaye ni mtoto wa John Riber ambaye ndiye aliyetayarisha filamu ya Neria (1993) na kuongoza Yellow Card (2000). Filamu ilipata kuchaguliwa katika kinyang'aro cha tuzo za ZIFF huko Zanzibar mwaka 2011. Vilevile filamu imeshinda tuzo ya "Golden Hamster" huko nchini Marekani katika tamasha la filamu la Northwest Projections, mjini Washington. Filamu ilipata kuteuliwa katika matuzo kemkem kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kutolewa. Filamu ilizinduliwa rasmi tarehe 4 Juni, 2011 katika viwanja vya BIAFRA ambapo kulikuwa hakuna kiingilio. (from Wikipedia, CC BY-SA)

More like this

This page is from Underplayed Gems. Not quite it? Tell the Catbot what you feel like watching and it picks from the whole catalogue, or browse by genre, country and year.

Lists: Korean thrillers worth the evening · Anime films beyond Studio Ghibli · Slow films for a rainy night · Horror that unsettles instead of startling · Series you can finish in a weekend · Nordic crime worth the subtitles · Good films that end in under 90 minutes · Documentaries that play like thrillers

Loading movies…

What should I watch?